Author, Cardia Lukando
Email, lukandodia@gmail.com
KIFUA 01
Ilikuwa asubuhi na mapema katika kanisa la mtakatifu Gasper lililoko mbezi beach, Harrison Mwakalinga alikuwa ni mwenye furaha sana kwa sababu ni siku ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake Veronica Oscar,Amependeza sana. Ndugu jamaa na marafiki wakahudhuria siku hiyo kuwapongeza wapendwa wao wakiwa wamependeza sana ,lakini muda ulizidi kwenda bila ya wao kumuona bibi harusi.
Mwanzoni hakuna aliyekuwa na mashaka juu ya kuchelewa kwa biharusi lakini kadri muda ulivyozidi kwenda hofu zilizidi kutanda. Watu walianza kutoka nje ya kanisa baada ya kuchoka kusubiri ndoa ifungwe,
"Mhh jamani,huyu Veronica anataka kucheza na akili za watu?"."We acha tu,yaani watu wanafanyaga matukio,siku ya mwisho ndo anaharibu,ona mwenzie anavyomsubiri kwa furaha,afu yeye ndo unakuta haji". Ilikuwa ni minong'ono ya baadhi ya watu,ilifika majira ya saa tano wazazi wa Harrison walionekana kupata wasiwasi kwa sababu walialika wageni wengi." Harris nini kinaendelea mbona mpaka sasa Veronika hajafika?" aliuliza mama mzazi wa Harrison ambaye alikuwa na wasiwasi sana,"Sijui mama!hata sijui na simu yake haipokelewi kwasasa..." Harrison alijibu huku akionekana kutokuwa na amani. Padre pamoja na watumishi wake waliamua kuendelea na ratiba ya kupokea watu wengine ambao walikuwa na ratiba ya kuingia kanisani kwa ajili ya kufunga ndoa.
Watu walianza kutawanyika,wenye magari yao na hadhi zao waliamua kuondoka,kwenda kuendelea na shughuli zingine lakini Harrison pamoja na wazazi wake na baadhi ya ndugu wa Veronica waliokuwa eneo hilo nao pia walibaki wakihangaika kupata taarifa za ndugu yao. Wapo baadhi ya marafiki wa Harrison waliomfariji kwasababu hakuwa sawa."Sijui niseme nini Harrison lakini jaribu kuwa mvumilivu huenda amepata dharula.." alisema rafiki yake aliyeitwa Daniel Damian. Ghafla simu ya Harrison iliita namba ilikuwa ngeni alipokea haraka na kusema "halloo..", "hellow bila shaka naongea na Harrison!" ilisikika sauti nzito sana ya kiume,"Yeah.. Ndio mimi, nani mwenzangu?" mtu huyo alikwepa swali aliloulizwa na kujibu "kuna ajali mbaya sana ya gari la bibi harusi imetokea hapa Ally Sykes road" Harrison alijikuta katika hali ya mshangao iliyofanya watu washtuke baadaye kusema mshangao mkubwa"What?!!" hiyo ilifafanya mama yake kumuuliza na "Nini kinaendelea Harrison?!" Harrison hakuwa sawa aliamua kuondoka haraka bila kumjiibu chochote mama yake. Alitoka haraka na kuelekea parking ya magari,na kupanda gari yake aina ya Harrier modern,aliitoa speed gari hiyo na kuanza kushika njia iliyoelekea barabara ya ndafu road ambayo haikuwa na magari mengi hivyo Harris aliovertake magari makubwa yaliyokuwa mbele yake Jambo ambalo ni hatari na ni kosa barabarani lakini akili yake ilishajaa mashaka juu ya Veronica,alikunja usukani na kutokea hekima road akizidi kukanyaga mafuta na suti yake nyeupe iliyomkaa vizuri sana mwilini akiwa smart,alikuwa speed sana na alizidi kuvunja sheria barabarani mpaka alipojipenyeza njia fupi ya kuingilia ya Ally Sykes road..
Mara baada ya kuingia barabara hiyo alishuhudia ambulance ikiwa imezungukwa na watu wengi lakini pia gari ya bi harusi ilikuwa katika hali ya kuharibika vibaya mnoo.. Harrison alifunga brake iliyofanya tairi za gari zitoe mlio mkali na chembe za cheche juu ya ardhi hiyo ya lami, watu walishuhudia na kumshangaa Akashuka haraka sana akikimbilia alipo Veronica,hapo ndipo alishuhudia dereva wa gari akilazwa kwenye machela akiwa na damu nyingi sana.. "Veronica?!"Harrison aliita kwa uchungu baada ya kumuona mpenzi wake alievalia shela nzuri lakini akiwa na hali mbaya sana kwani ametapakaa damu usoni,mwilini na mpaka kwenye shela,Harrison alimuwahi Veronica na kumshika kwa kumuita akiwa anaburuzwa na machela hana fahamu zozote
"Vee!!Vee wake up!".Aliita Harrison akitaka wamuache kwanza lakini Kikosi cha afya ambacho kilikuwa kikitoa huduma hiyo ya kwanza ya kuokoa maisha ya watu,kilimtuliza Harrison ambae tayari ametapakaa damu kwenye suti yake kwa kumkumbatia Veronica na haraka sana wajeruhiwa walipakiwa na kuwahishwa hospitali kubwa ya Taifa.
Sapnah Mohammed amejawa tabasamu kwa mpango wake kwenda sawa kama alivyotaka "kazi nzuri sana Erick, endeleeni kupata access zoote kuhusu Veronica.." " sawa madam ondoa shaka." Hivi ndivyo Sapna na Erick walivyozungumza kwa njia ya simu.. Sapnah alionekana mwenye furaha sana baada ya mpango wake kwenda sawa, alijipongeza kwa glasi ya Whine chumbani kwake.
**** ***** ***** ******
Veronica ni mwenye furaha sana kwani ni siku ambayo anafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu sana kwa jina la Harrison,
Veronica akiwa saloon akikarabatiwa kwa ajili ya siku yake maalumu,hakuchelewa sana baada ya kukamilisha huduma za saloon na kupendeza sana,Dada yake kipenzi Leticia alihakikisha anakuwa nae karibu mpaka mwisho,kisha akampeleka lilipopark gari lake lililopambwa vizuri " Harrison anakusubiri kanisani hivyo unapaswa kuwahi shoga angu!" alisema Leticia akimrekebishia shela vizuri mdogo wake tena kwa furaha."Naomba usichelewe Leticia unajua mimi mdogo wako sijazoeaa.." Veronica alisema akionekana kuwa na furaha ya uoga"Hahahaha kuzoea nini wewe nae?leo siku yako usiogope,ila siwezi kuja bila kurembwa banaa,shemeji yakoTony atanishangaa..."
Letcia alisema akimtania na kumsisitiza mdogoake kutangulia na hapo ndipo Veronica alianza safari ndani ya gari aina ya BMWx6.
Dereva alikuwa katika mwendo wa wastani mpaka walipoingia njia ya Ally Sykes road wakati safari inazidi kusonga mbele kuna gari kubwa aina ya Fuso ilitokea upande wa kushoto kwa kasi na kuwagonga, kitendo hicho kilifanya dereva pamoja na Veronica wapoteze mwelekeo,wote wawili walishangaa kwa nini gari hilo limewavamia namna hiyo..mbaya zaidi ni gari kubwa,lilifanya wakaanza kutoka nje ya barabara na kubamiza tena gari hiyo na kufanya Veronica apige ukelele mkali wa hofu kwani hali ilitisha lakini barabara hiyo ilikuwa kimya sana.
"Mungu wangu!!nini hiki!?"Alisema Veronica akihangaika na shela lake huku akianza kufungua mlango ajitupe nje."Toa loki nishuke basi!". "Hapana!hiyo ni hatari sana!utakufa!".
dereva alizidi kumsihi Veronica atulie kwani Veronica alizidi kulazimisha mlango ufunguke.
"Hii hali sio ya kawaida,nadhani kuna watu wamedhamiria kutuua!"alisema dereva kwa hofu kubwa,kwani alipojaribu kukwepa gari na kufunga breki pembeni lakini Fuso hilo liliifuata karibu na kuibamiza BMWx6 upande wa mbele kwenye boneti na kuisukumiza vibaya BMW na kufanya gari ipinduke na hapo hazikusikika tena kelele za Veronika wala dereva kuomba msaada kwani gari yao ilikuwa limepinduka na kuharibika vibaya sana.
Baada ya tukio hilo fuso lilitoweka na kuacha vumbi jingi,watumiaji wachache wa barabara hiyo walibaini Kuna ajali baada ya kuona gari lilioonekana kwa mbali limepinduka na kuharibika vibaya.
**** *** *****
Leticia alishtukizwa na taarifa hizo mbaya sana ndugu yake
Veronica kupata ajali mbaya..sio yeye tu,pamoja na mama yao aliewahi haraka hospitali.
Harrison ametapakaa damu anakimbiza machela aliyolazwa Veronica akiwa na mpira wa Oxygen puani iliyopokelewa na manesi "Veronica promise me you will be fine my love!!"( Veronica niahidi utakuwa sawa mpenzi wangu!!)watu waliopishana nae walimshangaa sana, Harrison aliongozana machela hiyo wakiwa katika hali ya kuchanganyikiwa mpaka mlango wa ICU,na hapo ndipo manesi walimzuia akionekana kutaka kuingia lakini milango ilifungwa akaachwa nje akizidi kuvurugika akili.
Ndugu kadhaa waliweza kuungana hospitali na wote walitaka kujua hali ya Veronica na dereva,wakiwa kwenye benchi alipita mmoja wa madaktari ambaye alikuwa akitoa huduma kwa dereva wa Veronica,aliweza kuvua miwani "docta hali ya mgonjwa ikoje?" aliuliza baba yake Harrison Mr Mwakalinga."Nasikitika kusema kwamba mgonjwa wenu amefariki kabla ya kufika hospitali"jibu lilimshthua kila aliekuwa hapo." doctor vp hali ya Vero...yuko sawa?!". Aliuliza Leticia akiwa katika hali ya hofu."Bado anapata matibabu naombeni muwe wavumilivu!."daktari aliondoka na kuwaacha.
Ni siku ngumu sana kwa Harrison kuliko watu wote kwani hakupata nafasi ya kumuona Veronica, kama zilivyo taratibu za hospitalini, ulifika muda ambao watu hawakuruhisiwa kuendelea kuwa hospitali wala kuwaona wagonjwa hivyo walilazimika kurudi nyumbani kila mmoja akisali sala yake kwa ajili ya Veronica.
Usiku huo katika chumba cha ICU alicholazwa Veronica,alitoka daktari ambaye aliemaliza kumfanyia huduma ya muda huo lakini kuna mtu alitokeza maeneo hayo akiwa amevalia barakoa nyeusi,kofia nyeusi na koti jeusi aliyeonekana kuwa makini sana kusubiri daktari atoke,daktari alipotoka mtu huyu aliye ficha uso wake alianza kuelekea usawa wa chumba alicholazwa Veronica na alipofika mlangoni alinyonga kitasa taratiibu na kuingia.Je nini kitaendelea?
0 Comments